Serikali imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia
Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza
kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana
kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya upinzani haitashiriki.
Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo bungeni kuhusu Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Serikali imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya upinzani haitashiriki.
Ofisi ya Rais
Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo bungeni kuhusu Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Serikali imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya upinzani haitashiriki.
Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo
bungeni kuhusu Makadirio ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
“Hatuwezi kuingia uchaguzi wa vitongoji, vijiji na
mitaa kwa utaratibu uliopo leo, hatuwezi kwenda kwenye Uchaguzi Mkuu
mwakani na Tume ya Uchaguzi kama ilivyo leo, hatuwezi tena kwenda kwenye
Uchaguzi Mkuu mwakani wakati matokeo ya uchaguzi wa Rais hayawezi
kuhojiwa mahakamani.”
Aliongeza: “Hatuwezi kuingia kabla na hoja ya
mgombea huru haijapatiwa majibu, tukiwa na daftari la wapigakura
lililopo leo na hatuwezi kulikubali daftari jipya litakalotengenezwa
kama wadau wote hatutashirikishwa kikamilifu.”
Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku moja tu baada ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwasilisha bungeni, Bajeti ya ofisi yake
ambayo imetenga Sh5 bilioni kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa
uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Mbowe alisema kama ilivyo kawaida, Serikali na CCM
inaweza kupuuza tahadhari hizo na kulazimisha kwenda katika chaguzi
hizo katika mazingira ambayo hayana mwafaka kama inavyoonekana sasa
katika Mchakato wa Katiba Mpya.
Ukawa haitarejea bungeni
Katika hotuba hiyo iliyobezwa na wachangiaji wa
CCM kuwa imezungumzia Katiba badala ya Bajeti, Mbowe alisema wajumbe wa
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hawatarejea katika Bunge la Katiba
mpaka watakapohakikisha kuwa maana halisi ya uwepo wa Bunge hilo
unafuatwa.
Alisema kama lengo ni kutumia mwavuli wa Bunge
Maalumu la Katiba ili kuendeleza mfumo wa kikatiba na muundo wa muungano
uliopo sasa, wajumbe wa Ukawa hawatakuwa sehemu ya usaliti huo kwa
Watanzania.
“Kama kitakachojadiliwa katika Bunge la Katiba
kitalenga kuboresha matakwa ya wananchi kama yalivyodhihirishwa katika
Rasimu ya Katiba na taarifa za tume, wanachama wa Ukawa watakuwa tayari
kurudi kwenye Bunge Maalumu la Katiba ili kuendelea na mjadala wa
rasimu,” alisema Mbowe.
Ofisi ya Rais
Mbowe alisema kati ya wajumbe 201 wa Bunge la
Katiba walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, zaidi ya wajumbe 160 ni
wanachama wa CCM.
Alisema hofu ya Kambi ya Upinzani kwamba CCM ingetumia mamlaka
ya Rais katika uteuzi wa wajumbe wa bunge hilo, sasa imedhihirika wazi.
Alisema wajumbe hao walichomekwa kwenye Bunge
Maalumu kwa kutumia kivuli cha waganga wa jadi, taasisi za kidini, asasi
za kiraia, taasisi za kitaaluma na watu wenye malengo yanayofanana.
“Hatua hii imechangia kujenga mazingira ya kutokuaminiana na hivyo kuweka msingi mbaya wa mchakato husika,” alisema.
Alisema hata lilipoanza Bunge la Katiba, CCM
iliendelea kufanya hila za kuchakachua kanuni za Bunge la Katiba ili
kupitisha hoja zao kirahisi.
“Walipoona wamekwama walimtumia Mwenyekiti wao
Taifa (Rais Kikwete) ambaye alitumia kivuli cha urais kusisitiza msimamo
wa CCM na kutisha wajumbe wa Bunge la Katiba kwamba kama ukipita muundo
wa serikali tatu jeshi litapindua Serikali,” alisema Mbowe.
Alisema Rais Kikwete ndiye aliyebariki uandikaji
wa Katiba Mpya Desemba 2010, lakini hivi sasa anaongoza mawaziri wake,
viongozi waandamizi, wabunge na wajumbe wa CCM kujadili Rasimu ya Katiba
kwa kutukana, kudharau, kubeza, kuzomea na kushutumiana.
Alisema kitendo hicho kinathibitisha kauli
zilizowahi kutolewa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina
Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema
kwamba Serikali ya CCM haioni haja ya kuwa na Katiba Mpya kwani iliyopo
sasa inatosha.
Credit: Mwananchi
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment