Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua ameziingiza katika njia ya haja kubwa.
Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema
mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na
baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa
Mahakamani.
Mwezi
March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo
walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75
za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano
wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za
kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment