Friday, May 9, 2014

Rais wa Urusi Vladmir Putin amewasili Sevastopol katika jimbo la Crimea lililojitenga majuzi kutoka Ukraine.


Awali katika guaride la heshma ya wapiganaji wanajeshi walioishinda jeshi la Ujerumani katika vita vya pili vya dunia Putin, aliusifu uzalendo wa majeshi ya Urusi na moyo wao wa kijitolea kwa uhuru wa taifa lao.


 
Putin akiwahutubia maelfu ya majeshi alisisitiza kuwa ni jambo la kujivunia na la uzalendo kulinda hadhi ya taifa .

Putin aliyasema hayo licha ya kuwa na taharuki kati ya mataifa ya magharibi na Moscow kufuatia hataua ya Urusi kutaifisha jimbo la Crimea kutoka Ukraine.

Zaidi ya wanajeshi elfu 11 wanashiriki guaride hiyo, huku wakiwa na zana za kivita zikiwemo vifaru, mizinga na ndege za kivita.

Sherehe kama hizo za ushindi wa utawala wa Sovieti katika vita vya kwanza vya pili vya Dunia zinaandaliwa katika mji wa bandari wa Sevastopol ulioko Crimea.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema kuwa litakuwa jambo la huzuni kwa bwana Putin kutumia maadhimisho hayo kwenda Crimea.

Hayo yanajiri huku habari kutoka Ukraine zikisema kuwa kumetokea vifo vya watu kadha katika mji wa Mariupol baada ya makabiliano baina ya mejeshi ya Ukraine na wapiganaji waasi wanaounga mkono Urusi.

posted by BBC >>>

0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!