Ndugu yangu msomaji wa habari hii, kwanza nakuomba unisamehe kwa kupost picha hii yenye kutisha, lakini sikuwa na jinsi ya kufanya imenibidi nikaiweke ili ujionee tukio zima lilivyokuwa.
Tukio hili la kusikitisha limetokea kwenye maeneo ya Buzuruga ambapo kijana mmoja ambaye alikuwa amebebwa katika pikipiki amejikuta akipoteza maisha yake baada ya zile haraka haraka za dereva wa bodaboda kutaka kuwahi ikabidi dreva huyo mwendesha bodaboda avunje sheria za usalama barabarani.
Baada ya kuvunja sheria ndipo alijikuta akiovateki roli kubwa ambalo mteja wake huyo alijikuta akinasa kwenye roli hilo ubavuni, sababu ya kunasa kwenye roli hilo nikutokana na kwamba kijana huyo alikuwa amebeba kibegi kidogo mgongoni mwake ambacho kilikuwa ndicho chanzo cha kunasa kwake.
Kijana huyo alijikuta akiingia kwenye uvungu wa roli hilo na ndipo dimbwi la damu pamoja na umauti ukawa umemfika pale pale alipokuwa.
kiukweli kijana huyo hakuweza ata kuomba maji ya kunywa zaidi ya roho yake kutoweka na huku akiacha damu ikitapakaa kama maji kwenye eneo la tukio.
Kiroho tupo nae lakini kimwili hatutomuona tana kijana huyu, sikubahatika kulijua jina lake mapema ila kwakuwa sote ni binadamu na wote ni ndugu hatuna budi basi kumuombea afike salama uko aendako.
tumuombee ili aweze kupokelewa vyema mbele ya Mungu wake, Mungu ailaze roho ya marehemu milele maari pema peponi.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment