Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi Jenerali
Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ wakiangalia vitabu
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya
Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu
jijini Dar es Salaam, Ijumaa Januari 9, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya vitabu
na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais
Kikwete amekabidhi vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha
Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar
es Salaam, Ijumaa Januari 9, 2015. Rais kikwete, ambaye
ameshachangia jumla ya vitabu 2752 katika maktaba ya chuo hicho na chuo
cha Monduli katika vipindi tofati, amesema elimu imo vitabuni, na ili
kuelemika
yapaswa mtu asome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa na vitabu.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange alipokuwa akimjshukuru kwa kutoa
vitabu 2752 kwa Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za JWTZ wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha
Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar
es Salaam leo Ijumaa
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkuu
wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ
baada ya hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya
Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu
jijini
Dar es Salaam, Ijumaa Januari 9, 2015.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment