John Haule (35) mkazi wa Lupapila Manispaa ya Songea amefariki Dunia
ghafla wakati akifanya mapenzi nyumbani kwa mpenzi wake jina
linahifadhiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 17 mwaka huu majira ya saa 8 usiku huko katika kijiji cha Subira manispaa ya Songea.
Alisema kuwa siku ya tukio Haule alienda nyumbani kwa mpenzi wake majira ya saa 2 usiku akitokea hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alikwenda kwaajiri ya kumuuguza mjomba wake na alipokuwa hospitali alimuaga mjomba wake kuwa amemkumbuka mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi 11.
Kamanda Msikhela alieleza zaidi kwa mjomba wake alimruhusu kurudi nyumbani lakini Haule akufika nyumbani kwake badala yake alipitiliza hadi nyumbani kwa mpenzi wake ambapo alipofika aliandaliwa chakula lakini marehemu alikataa chakula hicho kwa madai kuwa ameshakula alikotoka hivyo ilipofika majira ya saa 3 usiku waliingia chumbani kulala na kushiriki tendo la ndoa mpaka majira ya saa 5 usiku ambapo walipumzika huku wakijadili mahusiano yao.
Alisema kuwa ilipofika majira ya saa 8 usiku Haule ambaye ni marehemu alimuomba mpenzi wake warudie tena tendo la ndoa ambapo mpenzi wake alikataa akidai kuwa amechoka lakini baada ya kumlazimisha alikubali, ndipo akiwa kwenye tendo hilo Haule alisikika akitoa sauti ya kukoroma na kuanza kutetemeka jambo ambalo lilimshtua mpenzi wake huyo ambye alichukua jukumu la kwenda kuwaita majirani zake pamoja na mjumbe wa serikali ya mtaa, Winney Mwingira ambaye naye alitoa taarifa katika kituo kikubwa cha polisi cha mjini Songea.
Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa walienda eneo la tukio wakiwa wameongozana na Dkt. Ambaye alithibitisha kuwa Haule ameshafariki dunia na kwamba jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa upepelezi.

- STEPHANO MANGO: AFARIKI AKIFANYA MAPENZI SONGEA
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment