Mahakama Kuu nchini Misri jana Jumamosi ilimfutia mashitaka ya mauaji
rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak, mashitaka ambayo yalikuwa
yanamkabili awali yaa vifo vya waandamanaji wakati wa vuguvugu la
mapinduzi ya mwaka 2011 baada ya kujaribu kutaka kusalia tena madarakani
huku akiwa ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30.
Uamuzi huo umechochea hasira ya wapinzani wa Mubarak ambapo karibu watu 1,000 walikutana katikati mwa jiji la Cairo kupinga serikali.
Wizara ya afya imesema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia wakati Polisi wa kutuliza ghasia nchini Misri wakijaribu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi ya mahakama nchini humo.
Aidha mahakama imemwondolea rais huyo wa zamani mashataka ya rushwa, lakini ataendelea kubaki kizuizini kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kesi nyingine ya rushwa.
Maaafisa wengine saba waliohudumu kwenye serikali ya Mubarak akiwemo waziri wa zamani wa mambo ya ndani anayeogopwa Habib al Adly pia wamefutiwa mashitaka ya mauaji ya watu 800 waliouawa katika mapinduzi hayo.

via RFI Swahili
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment