Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.
Uongozi wa Kisiwa cha Jimbo la Hainan Nchini Jamuhuri ya Watu wa China
iko tayari wataalamu na awekezaji wake kufungua milango ya uwekezaji
katika Visiwa vya Zanzibar katika miradi ya Kilimo, Utalii na Mazao ya
Baharini kwa lengo la kusaidi maendeleo ya Zanzibar.
Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake ambao umenza ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku Kumi katika Jimbo hilo hapo Hoteli ya Le Meriden Mji Mkuu wa Kisiwa hicho wa Haikou.
Bwana Jiang Dinmgzhi alimueleza Balozi Seif kwamba Jimbo hilo ambalo ni Kisiwa kiliopo ncha ya Kusini mwa China limekuwa na utajiri mkubwa wa wataalamu wa Sekta hizo ambao unaweza kusaidia maendeleo na uchumi wa Zanzibar.
Alisema Uongozi wakeutaandaa utaratibu na mipango ya kusaidia kutoa taaluma ya kisasa kwa wavuvi na wakulima wa Zanzibar ili wapate fursa ya kuzalisha kitaalamu miradi yao hali itakayowaongezea kipato na kupunguza umaskini.
Gavana Jian Dingzhi halifahamisha kwamba hatua hiyo italenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Hainan Visiwa vinavyolingana na kufanana kimazingira.
Alielezea faraja yake kuona kwamba Kizazi kipya cha jamii ya Wananchi wa Jamuhuri ya Watu wa China kimekuwa kikijifunza uhusiano wa kidugu unaoendelea kuimarika baina ya pande hizo mbili.
Gavana huyo wa Jimbo la Hainan aliwashauri na kuwaomba wafanyabiashara wa Zanzibar kulitumia soko la Hainan hasa lile la mazao ya Baharini katika kuendeleza biashara zao.
Alisema Hainan imekuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya Baharini yanayokadiriwa kufikia Tani 50,000 ndani ha mwaka huu wa 2014.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Sekta za Kilimo, Utalii na Mazao ya Baharini zimekuwa zikitoa mchango kuongeza mapato ya Taifa.
Balozi Seif alimueleza Gavana Jian Dingzhi kwamba ziara ya Ujumbe wake ndani ya Jimbo la Hainan itatoa fursa ya kujifunza maendeleo yaliyopatikana ambayo yameliwezesha Jimbo hilo kupata ufanisi mpana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa shirika la Ndege la Hainan kuanzisha safari za moja kwa moja za usafiri wa anga kati ya Visiwa hivyo kwa lengo la kupanua wigo wa biashara hasa utalii.
Alisema uamuzi huo endapo utafikiwa unaweza kutoa nafasi kwa wawekezaji wa Hainan kuhamasika na hatiame kuamua kuwekeza miradi yao ya kiuchumi katika Visiwa vya Zanzibar.
“Ziara yangu hii pamoja na mambo mengine ya ushirikiano na uhusiano kati ya Zanzibar na Hainan lakini pia imelenga kushawishi wafanyabiashara na wawekezaji wa Hainan kuwekeza vitega uchumi vyao Zanzibar “.Alisema Balozi Seif.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake walitembelea meneo huru ya uwekezaji pamoja na kuangalia uzalishaji katika kiwanda cha usindikaji Samaki kwenye mji wa Kisiwa cha Haina, Haikou.
Akizungumza na wawakilishi wa Kiwanda hicho na ule wa Maeneo huru ya uwekezaji wakiongozwa na Meya wa Mji waChengmai Bwana Zhaomin Ji , Balozi Seif aliwapongeza Wananchi wa Hainan kwa hatua kubwa waliyofikia katika kuimarisha maendeleo yao.
Balozi Seif maendeleo hayo yanatoa nafasi kwa Zanzibar kujifunza kupitia ziara za mara kwa mara za viongozi na watendaji wake.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha maeneo huru ya uwekezaji pamoja na mfumo wa Bandari huru ya kiuchumi ili kuimarisha maendeleo yake lakini bado miundombinu katika maeneo hayo yangali duni.
Naye Msaidizi wa Meya wa Mji wa Chengmai ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Kamati ya Chama ya Mji huo Bwana Sitao Yang alisema Hainan ni miongoni mwa Majimbo yenye rasilmali kubwa ya kiuchumi ikitanguliwa na Taiwan.
Alisema uchumi wa Jimbo la Hainan umekuwa na kufikia uwekezaji wa Yuan Bilioni 20 mwaka huu kutokana na kuimarika kwa miundo mbinu yake inayotoa fursa katika uwekezaji wa sekta ya Utalii.
Bwana Sitao alimuhakikishia Balozi Seif kwamba juhudi zitaongezwa katika kuona uhusiano wa kidugu naendelea kuimarika kati ya Zanzibar na Hainan kwa kuweka ubia katika miradi ya kiuchumi na maendeleo.
Wakati wa Jioni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake walijumuika pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Tato wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye chakula cha jionikilichoandaliwa na Gavana wa Hainan Bwana Jian Dingzhi hapo kwenye Hoteli ya Le Meriden Mjini Haoku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha Uwekezaji wa Mji wa Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea ukumbi wa mkutano kwa mazungumzo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd. Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo haji.
Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa shati jeupe Bwana Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kushoto yake wakati ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo ukiwa katika ziara ya siku 10 Jimboni Hainan
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa vyakula vya viungo {spices} Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian, Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao rasmi wa
ushirikiano.
Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.(Picha na Hassan Issa, OMPR China)
- Picha, Maelezo, Habari: Othman Khamis, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (OMPR), China.
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment