Wakazi wa Mwananyamala wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI
wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa
eneo la mto Ng'ombe jirani na Rasco, Mwananyamala jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo.
Mtandao
huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi.
Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo
viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango
kujikinga na matatizo kama hayo.
"Nina
masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa
serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa
kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi
kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment