NJEMBA aliyejulikana kwa jina la
Mfaume Kassim amesurika kuuwa na wananchi wenye hasira kali baada ya
kutuhumiwa kuwalawiti watoto watatu wa kiume na kumbaka binti mmoja
(majina yao yanahifadhiwa) kwa nyakati tofauti.
Awali tukio hilo liliripotiwa kwenye Kituo cha Polisi Chanika na kufungiliwa jalada namba CHK/RB/718/2014 kabla ya kuhamishiwa Kituo cha Polisi Stakishari na kufunguliwa jalada namba STK/RB/3609/2014 KUBAKA.
Nyaraka zinaonyesha uhalifu uliofanywa na Mfaume Kassim.
Mjumbe wa Mtaa wa Kigezi, Mzee
Shabani alisema Mfaume aliokolewa na polisi waliofika eneo hilo lakini
wanakijiji wamefikia uamuzi wa kumfukuza kabisa kijijini hapo.
Binti aliyefanyiwa kitendo hicho kiovu cha ubakaji.
Tukio hilo lilitokea Chanika, nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi hao walifikia hatua ya
kumwangushia kipigo kwa madai kuwa, kila akikamatwa kwa vitendo hivyo,
huachiwa baada ya muda mfupi na kuendelea kudunda mitaani.
Akizungumza kwa uchungu baba wa mmoja
wa watoto waliofanyiwa kitendo hicho, Abdillah Mpacha (pichani),
alisema tukio lilitokea Kigezi, Chanika ambapo mtoto wake alikuwa
akitokea Madrasa.
Alisema, alipokuwa njiani kuelekea nyumbani alikutana na mbakaji huyo na kumlaghai kwa pipi na kashata kisha kumpeleka nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho.
Alisema, alipokuwa njiani kuelekea nyumbani alikutana na mbakaji huyo na kumlaghai kwa pipi na kashata kisha kumpeleka nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho.
Baba wa mmoja wa watoto waliofanyiwa kitendo hicho, Abdillah Mpacha akiongea kwa uchungu.
Hapa anafafanua zaidi: “Tulishangaa
kuona mtoto hana furaha kama kawaida, huku akiwa na wasiwasi mwingi,
baadaye akalalamikia maumivu ya tumbo.
“Tulipompeleka hospitalini, baada ya
uchunguzi na vipimo alionekana kuwa ameharibiwa vibaya sehemu za siri,
hapo ndipo akasema ukweli na kumtaja mbakaji akasema alificha kwa sababu
alimwambia kama angesema angemchinja.”
Alisema, kutokana na kuharibiwa sehemu za siri ilibidi awekewe mpira kwa ajili ya kujisaidia haja kubwa.Awali tukio hilo liliripotiwa kwenye Kituo cha Polisi Chanika na kufungiliwa jalada namba CHK/RB/718/2014 kabla ya kuhamishiwa Kituo cha Polisi Stakishari na kufunguliwa jalada namba STK/RB/3609/2014 KUBAKA.
Nyaraka zinaonyesha uhalifu uliofanywa na Mfaume Kassim.
Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo
wanasema kuwa, baada ya siku tatu, Mfaume alionekana nyumbani kwake
akiwa hana wasiwasi jambo lililowatia hasira na kuamua kumshushia
kipondo.
posted by paparazi >>>
0 TOA MAONI YAKO HAPA.:
Post a Comment