Saturday, April 19, 2014


Mnamo tarehe april 16 2014,Makamu mwenyekiti wa Bunge la katiba mjini Dodoma aliweza kuwatangazia wabunge matangazo ambapo moja ya matangazo hayo ni Hati ya muungano.Hati hii imeweza kupelekwa Bungeni baada ya kuzungumziwa sana na wajumbe mbalimbali hasa wanaotaka uwepo wa Serikali tatu.


Makamu mwenyekiti alisema,"nimepokea Hati ya makubaliano ya Muungano na certified copy na sasa nampa dakika mbili Mh.wassira atoe maelezo ya hati hii.
Mh.wassira alisema,"Juzi nilisimama katika Bunge hili na kusema kwamba Hati ya muungano iliyokuwa inapigiwa kelele, ipo katika hali nzurina ndani ya siku mbili itafikishwa bungeni.
Aliendelea kwa kusema,

"Sisi wote tumeapa na mwisho wa kiapo chetu tunasema ewe Mungu nisaidie,Mungu wa madhehebu yote ni mungu wa kweli na uongo ni kazi ya shetani,wamegawana kabisa Mungu wa kweli na Shetani wa uongo.

"Baada ya Hati kupatikana jana Tundu Lissu na wenzake wamekutana wakazungumza kwamba sasa tumesema sahihi ya karume sio sawa,tunaipeleka wapi Tanzania? yaani kila siku uongo unataka utawale Tanzania na ukweli upuuzwe?

"Watanzania tujihadhari na mawakala wa Shetani maana Mungu anatumia wanadamu kufikishia ujumbe wake kwa wanadamu wengine na shetani anatumia wanadamu pia,lazima tukwepe mamlaka ya Shetani na mawakala wao.

"mh.Tundu Lissu amewakashifu waasisi wa Taifa Mzee Karume na Mwl.Nyerere Mungu awaweke Mahali pema,anasema ni madiketa na waongo...!!! mimi nasema heshima ya viongozi wetu waasisi hailindwi na vyama,italindwa na Watanzania wote,wajibu wa kulinda heshima yao ni kwa woye. 

Hatuzuii mtu kusahihisha sera lakini huwezi kusema viongozi wetu ni waongo na madikteta,hatuna haki ya kuwakashifu,namwambia rafiki yangu Tundu Lissu,ulinzi wa heshima ya viongozi hawa ni wa Watanzania na utalindwa kwa gharama
yoyote....."




0 TOA MAONI YAKO HAPA.:

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!